Thursday, March 29, 2018

SIKILIZA NA TAZAMA NGOMA KALI KUTOKA KWA ALLY MIX


https://m.youtube.com/results?q=ally+mix+-+maua+sama&sm=1
[Continue Reading]

Monday, January 2, 2017

KIPA WA SIMBA ALIVYOCHAFUA DAFTARI


Golikipa wa Simba Daniel Agyei ameruhusu nyavu zake kutikiswa kwa mara ya kwanza tangu alipojiunga na klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili kuchukua nafasi ya Vicent Angban ambaye baadae alitemwa kwa kile kinachotajwa kuwa ni kiwango kidogo.
Agyei amecheza mechi tatu za ligi kuu Tanzania bara (Ndanda  FC 0- Simba, Simba 1-0 JKT Ruvu na Ruvu Shooting 0-1 Simba) na akifanikiwa kutengeneza clean sheets kwenye mechi zote. Alicheza pia mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Mtibwa Sugar (haukua mchezo wa mashindano rasmi) na kumaliza dakika 90 akiwa ameruhusu magoli mawili Simba ilipoteza kwa kufungwa 2-1.
Goli alilofungwa golikipa huyo kutoka Ghana lilitokana na kona ambapo beki wa Simba Novat Lufunga alijifunga wakati akipambana kuokoa mpira.
Kwahiyo Agyei ameruhusu goli moja hadi sasa katika mashindano rasmi yanayotambuliwa na TFF ukiondoa mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo aliruhusu magoli mawili katika kipigo cha Simba 1-2 Mtibwa Sugar.
Chanzo: http://shaffihdauda.co.tz/2017/01/01/golikipa-wa-simba-amechafua-daftari/
[Continue Reading]

Wednesday, July 15, 2015

HUYU YOUNG DEE HEBU ONA ANACHOKIFANYA HAPA


Msanii Young Dee amshika maungio msanii chipukizi Pvcombo,mashabiki wa mfananisha na Wema Sepetu 
video ya nyimbo yake!

 
[Continue Reading]

Tuesday, July 14, 2015

BARAKAH DA PRINCE _CHUKUA MUDA WAKO KUSOMA HAYA MASHAIRI YA WIMBO WA - SIACHANI NAWE


(verse1)
Wakati nalainisha moyo kupenda sio kama ninakosea
ipo sababu ya mimi kurejesha namba ambayo ilipotea
hali ya mtoto kumsusa mama akishachapwa
ni sawa na mapenzi
ukishapendwa
unasahau hata kama ulishafanyiwaga ushenzi
nakumbuka nilijuta sana kupenda kupenda kusikokua na thamani
ila hitaji la moyo lalazimisha kurudia zamani 



(chorus)
mimi bado nina imani
ipo siku utanipa thamani
mimi bado nina imani
jua me siachani nawe
na sishindani nawe
maana upo moyoni ndani
acha nisote mie
ila me siachani nawe
na sishindani nawe
maana upo moyoni ndani
wacha nisote mie

(verse2)
labda juu ya kaburi utanipenda mimi nikiwa sina uhai
hisia zangu haziheshimiwi najidharau sifai
heri ya upofu wa macho
kwa yale nayoyaona
umeruhusu mboni zangu me kumwaga machozi
yaani ungejua hisia za mapenzi
kutesa moyo ila bado hazichoshi
kupendwa sipendwi najua wazi ila bado silingi
maana kesho nitaurubuni moyo
unapendwa na unapenda me meno ila najiona kibogoyo
kweli penzi donda moyo

(chorus)
mimi bado nina imani
ipo siku utanipa thamani
mimi bado nina imani
jua me siachani nawe
na sishindani nawe
maana upo moyoni ndani
acha nisote mie
ila me siachani nawe
na sishindani nawe
maana upo moyoni ndani
wacha nisote mie
[Continue Reading]

WASANII WAIOMBA SERIKALI KUUMALIZIA UKUMBI WA BASATA

Wasanii nchini wameiomba Serikali kumalizia ujenzi wa ukumbi wa Sanaa za maonesho unaojengwa kwa zaidi ya miaka minane sasa makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) eneo la Ilala sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa ya Baraza hilo mapema wiki hii, wasanii hao walieleza kwamba kwa sasa kuna ufinyu wa kumbi za za maonesho hali ambayo imekuwa ikiwafanya wasanii hao kukosa maeneo ya kufanya sanaa zao hivyo kumalizika kwa ukumbi huo itakuwa ni ahueni kubwa kwao.

“Ukumbi huu ni muhimu sana kwetu, wengi tuliutazama kama mwanzo wa ufufuaji wa Sanaa za majukwaani lakini sasa ni muda mrefu hauoneshi dalili za kumalizika. Kuna kila sababu ya ukumbi huu kukamilika ili kutusaidia katika maonesho yetu” alisema Msanii Khalid Kambau.

Kwa upande wake msanii wa Sanaa za maigizo Christian Kauzeni ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wasanii waigizaji mkoani Dar es Salaam alisema kwamba kutokana na ukumbi huo kutazamwa kama mkombozi wa wasanii kuna kila sababu ya kuangalia mbinu mbalimbali ili kuhakikisha unakamilika mapema iwezekanavyo.

Awali akiwasilisha mada kwenye Jukwaa hilo la Sanaa iliyohusu ‘Ubora wa Filamu na Changamoto zake’ msanii na mzalishaji filamu maarufu nchini William Mtitu alisema kwamba tasnia ya filamu chini imepata umaarufu na kukua ingawa bado changamoto za uharamia, elimu na masoko zimeendelea kuiathiri.

“Kwa sasa filamu zinazozalishwa zimekuwa na ubora kuliko huko nyuma. Tatizo liko kwenye elimu kwa wasanii, uharamia na masoko. Kulikuwa na maduka zaidi ya sabini na tano yanayouza kazi za wasanii wa filamu lakini kwa sasa yamebaki sita tu. Wengi wameamua kuuza kazi za nje mbazo ni nafuu. Hii ni hatari” alisisitiza Mtitu.

Aliongeza kwamba pamoja na Serikali kuirasimisha sekta ya filamu bado kuna changamoto ya kazi zinazotoka nje kutokuwekewa stempu za mamlaka ya mapato huku kukiwa na uharamia unaotishia bei za filamu halali zenye stempu hizo.

Jukwaa la BASATA limekuwa likifanyika kwa mwezi mara mbili siku za Jumatatu na wiki hii kulikuwa pia na utambulisho wa asasi ya ubalozi wa Utamaduni wa Mwafrika ambayo imeasisiwa nchini Cameroon, Afrika Magharibi mwaka 2014.
Msanii na mzalishaji filamu nchini William Mtitu (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) wakati akiwasilisha mada iliyohusu ‘Ubora katika filamu na changamoto zake’ kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kushoto ni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli.
Rais na mwanzilishi wa asasi ya Mabalozi wa Utamaduni wa Mwafrika (African Culltural Embassy Association) Bwana Colpas Numfor kutoka nchini Cameroon (Katikati) akionesha nyaraka mbalimbali za usajili wa asasi yake wakati akiongea na wadau wa Sanaa kwenye programu ya BASATA ya Jukwaa la Sanaa. Kushoto kwake ni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli na Kaimu Mkurugenzi wa asasi hiyo nchini Tanzania Bw. Maganiko Charles.
Msanii maarufu wa Sanaa za majukwaani na maigizo Bakari Mbelemba maarufu kama Mzee Jangala akifuatilia kwa makini mjadala kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kushoto kwake ni Rais wa chama cha wacheza bao nchini Bw. Mande Likwepa.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyoibuka kwenye Jukwaa hilo la Sanaa.
Afisa Masoko kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Pastory John akitoa maelezo mbalimbali kuhusu urasimishaji wa sekta ya filamu nchini kwenye Jukwaa hilo la Sanaa.
Mdau wa Sanaa na utamduni Bw. Francis Kaswahili naye alitoa mchango wake kwenye Jukwaa la Sanaa. Alitoa wito kwa wasanii kuhakikisha wanakuwa na kauli moja katika kuhakikisha wanasimamia maslahi yao.
Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria Jukwaa la Sanaa wiki hii.
[Continue Reading]
Powered By Blogger · Designed By Seo Blogger Templates